Mtandao wa Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu kwa ufadhili wa African Women
Development Fund (AWDF) umeandaa mkutano wa siku mbili wadau wa haki za binadamu
wafanya maamuzi na mashirika ya utetezi wa haki za binadamu kujadili na kushauriana
fursa zilizopo za uwepo wa mazingira salama ya wanawake watetezi wa haki za binadamu.
Mkutano huo umekutanisha wadau kutoka serikalini na asasi za kiraia ikiwa ni pamoja na
Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Sheria na Katiba, Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Tume ya Kurekebisha Sheria. Mashirika Yasiyokuwa ya
Kiserikali ni kama WATED, WAHEAL, LHRC,
Protection International Africa. Mkutano huu unaendelea kufanyika kuanzia Leo tarehe 22 na 23 Mei 2024 mjini Morogoro.
Members Registered
Cases Intervened
Projects Completed
Copyright © CWHRDs-Tanzania