MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Mtandao wa Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (CWHRD) kwa kushirikiana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) hii leo umeungana na wanawake watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania kuadhimisha Sikukuu ya Wanawake Duniani. Maadhimisho hayo yaliyowakutanisha wanawake watetezi wa Haki za Binadamu zaidi ya Arobaini (40) yamebeba kauli Mbiu isemayo Wekeza kwa wanawake, Harakisha Maendeleo Mkurugenzi wa Mtandao wa Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania Bi. Hilda Stuart ambaye pia ni Katibu wa Mtandao wa Watetezi wa wanawake Afrika amekuwa miongoni wa Wazungumzaji wakuu na wandaaji wa Maadhimisho hayo ameeleza hali ya wanawake watetezi wa haki za Binadamu Tanzania na nafasi ya Mtandao katika kuhakikisha wanawake wanapewa nafasi ya kutekeleza shughuli za utetezi huku wakibaki kuwa salama. “Sasa hivi tunapigania haki za watetezi sababu kwa kipindi kirefu hata serikali ilikua haitambui uwepo wetu, Vitisho vimekua vingi kwa wanawake watetezi wa haki za binadamu mpaka sasa wanawake watetezi wengi wanaishia kuongea kupitia mitandao mbalimbali kupata suluhu ya uvunjwaji wa haki za binadamu” Ameongeza kwa kuwa nchi bado haina mifumo Thabiti ya kuwalinda wanawake watetezi wa haki za binadamu hii inapelekea watetezi wengi kupata vitisho vingi kutokana na kukosekana kwa mifumo hiyo.

IMETOLEWA NA MTANDAO WA WANAWAKE WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA 6 Machi, 2024

Big thank you to The Guardian Newspaper for shining a light on the important work of women human rights defenders in Tanzania. Donors play a crucial role in supporting the incredible efforts of organizations like CWHRDs TZ. Let's continue to invest in and empower these amazing women! Read More

Members

78

Members Registered

Litigation

2

Cases Intervened

Projects

5

Projects Completed

Copyright © CWHRDs-Tanzania