Mon - Fri : 09:00 - 17:00
Mtandao wa Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (CWHRDs Tanzania) umeadhimisha siku ya wanawake watetezi wa haki za binadamu duniani katika ukumbi wa hotel ya Sleepway jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Dr John Jingu katibu mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto. Maadhimisho hayo hufanyika kila tarehe 29/11 kuwakumbuka na kuwapa heshima wanawake wote watetezi wa haki za binadamu ambapo Mtandao uliwatunuku cheti wanawake vinara watetezi wa haki za binadamu. Waliotunukiwa vyeti ni pamoja na...
Katika maadhimisho hayo kulikuwa na mdahalo wa Unyanyasaji wa Kingono Mahali pa kazi ulioongozwa na Jackiline Tung'ombe wa shirika la PGWOCADE, huku wazungumzaji wakiwa ni Mery Rusimbi mkurugenzi wa shirika la Women Fund Truste Tanzania, Anna Kulaya Mkuregenzi wa WiLDAF, na Nabor Assey kutoka ofisi ya Tume ya Hakiza Binadamu na Utawala Bora Tanzania.
Pia kulikuwa na mdahalo wa mauaji ya wanawake na wapenzi ulioongozwa na Getrude Dyabane wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), wazungumzaji wakiwa ni Lulu Urio Mkurugenzi wa Shirika la Hodari, Wakili Anna Henga Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania, pamoja na Dr Evaristo Longopa kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu Tanzania.
Mdahalo mwingine ulikuwa ni Ukatili wa Kijinsia Mtandaoni pamoja na Udhalilishaji wa Wanawake na Wasichana. Mdahalo huu uliongozwa na Marcela Lungu Mkurugenzi wa TIBA Tanzania huku wachangiaji wakiwa ni Zaituni Njovu Mkurugenzi wa Zaina Foundation, Asteria katunzi kutoka shirika la TGNP.
Members Registered
Cases Intervened
Projects Completed
Copyright © CWHRDs-Tanzania