Muhanga wa ukatili

Mtandao wamsaidia muhanga wa ukatili

Mtandao wa Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu tukiwa pamoja na shirika la Door of Hope To Women and Youth, tumefika nyumbani kwa dada Fadina Musa Namponda muhanga wa ukatili wa Kijinsia aliyenusurika kuuawa na mumewe na kupata ulemavu wa kudumu wa kukatwa mikono baada ya mahakama kuamua kuwa mali alizochuma mwenyewe si mali za ndoa. Licha ya msaada wa mahitaji ya kila siku na gharama za kumfikisha hospitali kwa ajili ya matibabu, pamoja na mahali pa kuishi Mtarwa mjini akiwa anasubiri matibabu yake, Dada Fadina anahitaji kupata mikono bandia ili imuwezeshe kufanya shukguli ndogondogo na kupunguza utegemezi kwa watoto ambao wanahitaji kuhudhuria masomo shuleni. Michango ya Kununua mikono bandia ifikishwe kwa shirika la Door of Hope to Women and Youth lililopo Mtwara. Wasiliana na Mkurugenzi wa Shirika la door of hope kwa maelekezo ya kuchangia

Members

66

Members Registered

Litigation

2

Cases Intervened

Projects

2

Projects Completed

Flag Counter

Copyright © CWHRDs-Tanzania