Mon - Fri : 09:00 - 17:00
Mtandao wa Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania umetoa rai kwa umma juu ya mauaji ya kutisha ya wanawake yanayotokana na mahusiano ya wanandoa, wapenzi ama watoto wao. Rai hiyo imetolea leo tarehe 13/01/2022 kama ifuatavyo.
1. Vyombo vyote vya serikali ikiwemo Mh.Rais na Viongozi wote kutekeleza kwa vitendo Katiba na Sera na viapo vyao walivyoahidi kulinda watu na mali zao kwa kutoa ulinzi kamili kwa wanawake wote dhidi ya vitisho na mauaji. Kwa sasa Matukio haya yanaichafua nchi kwa kuashiria tunanyemelewa na uvunjifu wa amani.
2. Kamati za Ulinzi wa wanawake na watoto zifanye kazi kikamilifu kuibua migogoro ambayo ni tishio kwa maisha ya wanawake na watoto na kutoa taarifa kwa wahusika kuzuia madhira haya kwani ukatili huu hautokei siku moja tu, huanza taratibu na kuwa sugu.
3. Viongozi wa kiroho kusaidia kuelimisha waumini wao na kuwa msaada penye viashiria vya kifo na kuepuka misimamo hatarishi inayoweza kuwaletea hatari ya kifo waumini wao.
4. Wazazi na jamii kusaidia watoto wao wa kike wanapoleta mashauri hatarishi kwa maisha ya binti zao badala ya kusimamia au kutaka ama kuficha ukweli au kufurahisha jamii kwa kuwahimiza wavumilie mahusiano hatarishi kwa uhai wao.
5. Maofisa ustawi wa jamii wachukue jukumu la kuisimamia jamii kutatua matatizo katika jamii. wasaidie kutoa ushauri sahihi na kupeleka mashauri kwa wataalamu wa afya ya akili au vyombo vingine vya dola kwa msaada zaidi.
6. Eneo la afya ya akililiangaliwe upya kwa kuona jamii inapataje elimu ya kupunguza misongo ya mawazo kwa mtu mmoja mmoja na kuwa na uwezo wa kukabili msongo wa mawazo na si kuzihamisha kwa mwingine na kusababisha majeraha au vifo.
7. Madawati ya jinsia yaongeze uchunguzi na njia zaidi za kupambana kuzuia ukatili usifikie hatua za mauaji.
8. Kila familia ione ina wajibu kuchangia katika ulinzi wa watoto wao wa kike kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwani ni watu wa kwanza kujua hali tetekatika mahusianoya nduguzao hivyo kuwaokoa kwa wakati kutoka katika kifo.
9. Ifikie mahali wanajamii nao wachukue hatua za kuwalinda wanawake badala ya dhana ya kutoingilia mahusiano ya wenzi hivyo ata wanapoombwa msaada kwenye hatari wajitokeze klwa wingi kusaidia.
10. Wakati umefika wa kuwa na sheria inayokataza ukatili wa kijinsiainayojisimamia ili kukabiliana na changamoto zinazokithiri
11. Vyombo vya habari view chachu ya kuelimisha na kuibua matukio haya na kuichagiza serikali na wadau kuchukua hatua.
12. Sisi watetezi wa haki za binadamu pamoja na wanaharakati tuanzishe program kwa kushirikiana na serikali zitakazo kwenda moja kwa moja katika jamii ili kutatua changamoto za kijamii.
13. Watuhumiwa kuchukuliwa hatua stahiki, za kisheria kwa wakati, kwani tumeona kutokuchukuliwa hatua za haraka kwa watuhumiwa wa vitendo vya ukatili Mfano Mtuhumiwa wa aliyemkata masikio mwenza wake katika matukio aliyokuwa akiyafanya kwa wenza wake waliopita hivyo kupelekea vitendo hivyo kuendelea kwa kukithiri.
Members Registered
Cases Intervened
Projects Completed